Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa
jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa
kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya sita na
binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Debora Jacob.
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake,
lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha
Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya
rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.
Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la
Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye
gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya
kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
Fumanizi hilo lilikuwa limesukwa
na wasanii wa
kundi hilo kwa
lengo la kumkomoa
mzee huyo wa
kanisa ambaye alikuwa
ni mfadhili wa kundi lao
aliyeanza kutumia mgongo
wa ufadhili kuwatongoza
mabinti wa kundi
hilo mmoja baada
ya mwingine.
Wakiwa ndani ya gesti
hiyo, wasanii wa kundi
hilo walivamia chumba
hicho na kuanza
kumchomoa mzee huyo
ambaye aliruka ukuta na
kudondokea kwenye matuta ya viazi.
Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao
lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba
iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha
mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa
kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu
wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani
ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja
na kuomba ushauri.
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya
hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii
waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele
‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa
kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na
kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji
pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni
mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi
ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha
Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba;
RB/3843/2014
-RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI
YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
No comments:
Post a Comment