Hili ni bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha
Mdui kata ya Mawala wilaya ya Mtwara vijijini kwenye mkoa wa mtwara liliokotwa
na watoto waliokuwa wakicheza karibu na eneo la makaburi.
Taarifa ilitolewa Polisi baadaye ambapo baada ya wataalamu
kuja na kuchunguza waligundua ni bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba
TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618 ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la
Wananchi walichukua hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.
Kaimu kamanda wa Polisi Mtwara Maisha Maganga alikuwa na
haya ya kusema
kuhusiana na bomu
hilo:
"Ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu nadhani
ni kipindi kile cha vita ya Msumbiji, tulilipeleka porini likalipuliwa na
ulipuaji wake haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema
limeletwa ama imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu"
No comments:
Post a Comment