BONDIA Ibrahimu
Class 'King Class Mawe' amewashukuru viongozi wa ngumi nchini kwa sapoti yao
wanayo mpa tangu ahanze ngumi mpaka sasa kwani yeye malengo yake ni kufika
mbali zaidi baada ya
kunyakuwa mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na WPBF Africa Welterweight Title
Aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa DDC Keko kulipokuwa na mkutano
mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini cha TPBC, ambapo alikutana na viongozi
mbalimbali na kupongezwa kwa kunyakuwa mkanda huo wa ubingwa alioupata Zambia
kwa kumpiga bondia Mwansa Kabinga kwa TKO ya raundi ya tisa katika uwanja wa
Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia
bondia huyo
mwenye ndoto za kuwa mmoja wa mabondia watakotamba duniani ambapo mwanzoni mwa
mwaka huu aliteuliwa kuwa bondia bora wa mwaka 2013 katika uzito wake tuzo
zilizoanza kufanyika mwaka huu
fikra zake kwa
sasa ni kuwa bingwa wa mikanda mbalimbali inayotambulika Duniani katika uzito
wake fikra zake siku moja ni kupambana katika mapambano makubwa zaidi hususani
katika ukumbi wa MGM Gland nchini Marekani.
Bondia huyo
mwenye rekodi ya kushinda mapambano 11 na kupoteza mpambano mmoja wakati ananza
mchezo huo.bondia huyo anawashukurujopo la makocha wake wa kambi ya ilala
linalo ongozwa na kocha mkongwe wa mchezo huo Habibi Kinyogoli 'Masta',kondo
Nassoro,Sakwe Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mhamila 'Super D' kwa kumsimamia na kumpa ushari anapokuwa ulingoni akipambana
bila kuwasahau
mashabiki wake waliojaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na Tanzania nzima
kwa ujumla
No comments:
Post a Comment