Inawezekana hili likawa moja kati ya maswali uliyonayo na
hujawahi kupata nafasi ya kumuuliza muhusika au inawezekana ikawa ni ishu
ambayo umewahi kuisikia au kuisoma kwenye chombo chochote cha habari.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais
wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview
na millardayo anasema:
"Kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona
mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua
na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi.
"Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake
Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni
tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa
zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto mfano
kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au wanajitoa akili
katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi.
"Kuna kipindi unaweza ukashangaa Mwandishi wa habari
anachukua kalamu anaandika maneno mpaka unashangaa kayatolea wapi? sitaki
kuamini kwamba Mwandishi unaweza kuandika kwamba Ridhiwani kapata UNEC kwa
sababu ya baba yake, ungechukua muda ukamsoma Ridhiwani vizuri ukauliza watu
waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi kuwa kiongozi??.
"Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua Ridhiwani baada ya
Jakaya Kikwete kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo Ikulu lakini hawajui
Ridhiwani kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua anaishije, mimi nimekua naishi
maisha ya kawaida nimekaa boarding school nimesoma Mkwawa baba yangu akiwa
Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma Ulaya lakini nimesoma chuo kikuu Dar
es salaam pale japo nilikua na uwezo wa kwenda popote pale ninapotaka ila ni
kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona naishi kama watu wengine"
No comments:
Post a Comment