Monday, June 30, 2014

ALICHOKISEMA DIAMOND BAADA YA TUZO YA BET ALIYOKUWA AKIWANIA KUCHUKULIWA NA DAVIDO WA NIGERIA



Baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz aliyekua anawania pia tuzo hiyo ameandika ya moyoni kwa watu wake.
 
"Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo.

"Katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa.

"Cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi kunisupport"


No comments:

Post a Comment