Kufuatia Mahakama ya Ilala jijini Dar kumuachia
kwa dhamaa Emmanuel Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji wa nyimbo za
Injili maarufu nchini Flora Mbasha anayekabiliwa na tuhuma nzito za
kumbaka mdogo wa mkewe, inaelezwa kuwa siku moja tu aliyokaa
mahabusu ilimfanya kubadilika muonekano kutokana na
kudhoofika.....
Emmanuel Mbasha ambaye alifikishwa mahakamani kwa
mara ya kwanza juni 17 mwaka huu na kukosa dhamana kutokana na
kushindwa kutimiza mashariti, alilazimika kutupwa mahabusu katika gereza
la Keko, kabla ya juni 19 kupandishwa tena kizimbani ambapo aliachiwa
kwa dhamana baada ya kutimiza masharti hayo....
Baadhi ya watu ambao walimshuhudia Mbasha katika
viunga vya mahakama hiyo walioneklana kulengwa na machozi huku wengine
wakitamka kwamba wanamuachia Mungu.....
Mume huyo wa Flora aliwasikitisha zaidi watu
kutokana na kuwa na mawazo mengi huku miguuni akiwa amevaa malapa
ambayo thamani yake haizidi sh. 2000 wakati katika hali ya kawaida
huwa anavaa mavazi ya bei mbaya na kujiweka msafi muda
wote.....
"Maskini Imma amevaa ndala na amekonda.Hakika
yupo katika kipindi kigumu sana. Jela mtu hukonda siku moja tu.Jela
siyo kuzuri hata hata kidogo," alisema raia mmoja nje ya mahakama
hiyo.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Wilberforce Luhwago aliahirisha kesi hiyo hadi July 17 mwaka huu itakapo tajwa tena.....
Baada ya kuachiwa, Mbasha alitoka nje ya
mahakama hiyo kwa kasi na kuingia kwenye gari kisha kutoweka eneo
hilo....
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja kati ya
ndugu wa Mbasha ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kuwa mume
wa mwanamuziki huyo aliwaambia hana hamu na jela,
"Mbasha alisema kuwa jela hakufai kabisa na
alisisitiza kuwa asaidiwe kutoka kwa dhamana. Alisema siku moja
aliyoishi mahabusu ni kama mwaka mzima," alisema ndugu
huyo.
Aidha ndugu huyo alisema kwamba kitendo cha
Flora kutomtembelea mume wake ni cha kinyama na hakuna
aliyekitarajia.
"Hakwenda kumuona mume wake.Kwa kweli jambo
hili limetushangaza sana na kutuumiza sana, sijui mwisho wake utakuwa
vipi lakini tunaamini yatakwisha, kwa uzuri au ubaya,"
alisema.
Baadhi ya mahabusu ambao walikuwa selo moja na Mbasha katika gereza la Keko wamesema kwamba wamefurahi kuwa na nyota huyo kwani wamekuwa wakimsoma kwenye magazeti tu.
No comments:
Post a Comment