Wema Sepetu ameonekana kufungukia wale wanaomtukana kila siku na sasa kufikia hatua ya kumtukana hadi mama yake mzazi...
Kupita mtandao mmoja wa kijamii, Picha moja ya mama
mzazi wa Wema Sepetu iliyotengenezwa na kuwa CHAFU ilitolewa na kisha
kuanza kushushiwa matusi mazito...
Baada ya Picha na Matusi hayo, Wema amefunguka kwa
uchungu kwa kuandika:
"Dah...! Sijui hata niseme nini...! Ila si mlitaka kuniumiza... leo mmefanikiwa... nawapeni hongera.... Tena mmetisha haswa... Kila sjku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu... Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo...
"I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out
of it... Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo... Mzazi nwenyewe
ndo nimebakia nae mmoja tu... mnataka afe na yeye nibaki yatima sio... dah...
leo mmeniweza... saana jamani... Basi naomba isifike huko... nina uchungu sana
na mama angu ... nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama
angu...
"Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende
ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako... una mama wewe.. au uliokotwa na hujui
uchungu wa mama... dah... nime surrender leo.... hongera zenu narudia tena...
mmeniweza leo.... dah...
No comments:
Post a Comment