Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji
yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la
wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja siku moja baada ya kundi hilo
kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku na
kuua watu zaidi
ya 50.
Akitoa hotuba yake ya kitaifa, Rais Kenyatta pia amesema
maafisa wa polisi Mpeketoni ambao walifanya uzembe hadi kutokea mashambulizi
hayo watashtakiwa.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya habari
kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu jioni.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo na
kuua watu 20 licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa
washambuliaji walioshambulia Mpeketoni walikuwa wamerejea salama nchini
Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku
washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari
waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea
uhasama miongoni mwa jamii.
No comments:
Post a Comment