Serikali ya Kenya imewataka wananchi kuangalia mechi za michuano ya kombe la dunia katika maeneo ya majumbani badala ya sehemu za wazi zilizojazana na ambazo hakuna ulinzi.
Ushauri huo umetolewa kufuatia siku mbili za
mashambulizi katika mji wa Pwani wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu
60.
Mashambulizi hayo yalianzia katika eneo la Mpeketoni
ambako mashabiki walikuwa wakiangalia mpira siku ya
Jumapili.
Waziri wa usalama wa ndani amesema licha ya kuwa ulinzi
umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini, wamiliki wa baa na migahawa
wanatakiwa kuchukua tahadhari zaidi.
No comments:
Post a Comment