Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea
kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga
risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi
huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi
huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema
kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango
ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa
kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na
baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote
wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.
No comments:
Post a Comment