Baada ya kuonekana noti ya shilling mia tano ipo kwenye
mzunguko mkubwa kuliko noti nyingine zote hali inayo isababisha ichakae mapema,
huku kiwango chake cha kuhimili mizunguko kikiwa hakizidi miezi sita.
Benki kuu ya Tanzania inatarajia
kuibadili noti ya 500 kuwa sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika
July 2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo sarafu
ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki
na ubora wake uleule.
‘’Tunafanya hivi kwa sababu noti ya 500 inachakaa haraka
ukilinganisha na mzunguko wake na
kuwafikia watu wengi pia huchakaa haraka kutokuwa na mzunguko wa kushikwa na
watu wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya
wanaoshika za elfu kumi kwa siku,’’ alisema
mkurugenzi wa huduma za kibenki
wa BOT, Bw Emmanuel Boas katika maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment