Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kumekuwa na baadhi ya binadamu wachache ambao wamekuwa ni mahili sana kutumia umbumbumbu na udhaifu wa binadamu wenzao kuwadanganya na kujipatia kipato! mara nyingi watu hawa inasemekana wana kiwango kikubwa cha akili na ni wabunifu kupindukia... huwa tunawaita MATAPELI. hawa wapo kuanzia kule kijijini Namtumbo Ruvuma mpaka New York City, marekani! kwa mtazamo wangu wafuatao ni MATAPELI wakubwa zaidi kuwahi kutokea hapa nnchini ambao walitingisha na kuteka hisia za watu..
5. MANYAUNYAU
Huyu jamaa wote tunamfahamu, aliiitikisa sana miaka ya 2006,2007, na 2008! alijigamba kuwa akinywa damu ya paka anapata uwezo wa kimiujiza kufichua wachawi.! alizunguka mitaa karibia yote ya uswahilini hapa Dar, except huko udhunguni masaki n.k (sijui huko hakuna wachawi)! baada ya kuteka hisia za watu vya kutosha akaanza na ziara za mikoani... jamaa akaingiza mkwanja mrefu sana kwa kazi yake hii, nakumbuka miaka ile ya 2008 alinunua RAV 4 flani hivi kali sana, na mjengo wa maana.! sijui kwa sasa amepotelea wapi, inawezekana kazi yake ilikuwa effective wachawi wameisha!!!!!!
4. ALEX MASSAWE
3. DAUDI BALALI
Binafsi nahisi huyu ni moja kati ya watanzania ma-genius zaidi kuwahi kutokea! huyu kipindi anasoma alirushwa sana madarasa kutokana na kiwango kikubwa cha akili hii ikapelekea yeye kusoma elimu ya msingi na sekondari kwa miaka 10 tu!!! akiwa na miaka 18 alijiunga na chuo kikuu cha Howard, marekani ambapo alitunukiwa shahada yake ya kwanza. Akiwa na miaka 25 alitunukiwa PHD na chuo kikuu cha John Hopkins.!! kisha akarudi nchini kuwa mchumi wa benki kuu mwaka 1967. Baadae kidogo akaajiriwa IMF ambako alifanya kazi huko kwa miaka 23 kabla ya Mzee Mkapa kumrudisha nnchini kama mshauri wake wa masuala ya uchumi na baadae kumfanya Gavana wa benki kuu.! kinachofanya kumuweka Balali kwenye list hii ni tukio alilolifanya la ukwapuaji kiasi cha Bilioni 164 za kitanzania pale benki kuu! Nafahamu kuna theories nyingi sana kuhusu UFISADI WA EPA, lakini kwa mujibu wa serikali ni kuwa Balali alikula njama yeye binafsi na wale wafanyabiashara wakwakwapua fedha pasipo serikali kujua! kwa maana hiyo BAlali alimpiga changa la macho Waziri Mighiro, raisi, na hata usalama wa taifa! hivi ni binadamu wangapi wana uwezo wa kupiga mtonyo na mchongo mkali kama huu! Balali anaweza.....
2. DECI
Inawezekana hata wewe ulikuwa ni mmoja wa "waliopanda mbegu" DECI.!
Haya yalikuwa ni maumivu ya Taifa.! watu walipanda mbegu, mvua zikanyesha, lakini ghafla jua likawaka mavuno yakaingia mitini.. kuna watu wakisikia hili jina tu kichwa kinaanza kuuma.!
wanasema wajinga ndio waliwao, wenzetu huko udhunguni mfano marekani, huu mfumo wa DECI ulishapigwa marufuku toka miaka ya 1920, wenyewe wanauita PONZI SCHEME (PYRAMID SCHEME), lakini sisi kwetu ulikuwa ni mfumo mpya na watu waliona DESI nmkombozi tukakimbilia, wajanja wakatula alafu wakasepa kimya kimya! ila ilitufundisha tusipende bure bure..
1. BABU WA LOLIONDO
Mpaka leo bado sijaelewa Babu aliwezaje kutupiga changa kiasi kile! hivi ni kwamba babu alikuwa kichwa sana, au media ilisaidia! kipindi kile kuna watu walitamani Babu atangazwe kuwa nabii, au shujaa wa taifa! mpaka wakuu wa nchi walitengeneza mpaka kiwanja kidogo cha ndege wakawa wanatua, wanapanga foleni, wanapiga magoti kwa unyenyekevu kabisa na kuachama midomo kama wanakula sakramenti.! kila kona ilikuwa ni Babu, babu, babuuu..... kila mtu anapigania akanywe KIKOMBE! sijui hata ilikuwaje, maana ghafla tu, ziiiiii!! babu kimya! kila mtu kimya kimya akashtuka huu ni uzuzu.... lakini sio mbaya sana kwa jero jero tulizo mchangia babu! maana angalau sasa ana maisha yanayo eleweka na siha yake iko poa! naamini tutakuta 'thawabu' zetu huko juu..
No comments:
Post a Comment