SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,324
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na
uwezo
kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324 ambazo ni kwa ajili ya waajiri
mbalimbali
Nchini.Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334
zimeainishwa
bayana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ili
kuwawezesha
wahitimu wote wenye sifa na uwezo kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi
hizo
ajira Serikalini. "Nadhani ni vizuri zaidi kwa kila muhitimu anayetafuta
kazi serikalini
kufungua
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuangalia nafasi za kazi zilizotangazwa na pale
anapoiona
kazi inayoendana na sifa alizonazo kutuma maombi yake ili kuweza kushindanishwa
na
wengine....maana ajira za Serikali hivi sasa ni za ushindani hivyo inampasa
kila anayetaka
kupata
kazi serikalini kujiandaa vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya
kuajiriwa katika
Utumishi
wa Umma" alisema Daudi. Alifafanua kuwa kwenye tovuti
hiyo
kuna matangazo mawili tofauti ya kazi ambapo moja liko katika lugha ya
Kingereza likiwa
na
jumla ya nafasi za kazi 447 na tangazo lingine lipo kwa lugha ya Kiswahili
ambalo lina jumla
ya
nafasi za kazi 877. Aidha,
alizitataja
baadhi ya nafasi hizo za kazi zilizoko katika tangazo la kazi kwa lugha ya
Kiswahili
kuwa
ni Mhandisi kilimo (agro–engineers), Afisa kilimo (agro–officers) Mkufunzi
kilimo
(aquaculture),
Afisa kilimo msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary
officers),
Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer), Daktari mifugo mkufunzi
(veterinary
tutor),
Mkufunzi mifugo (animal science), Afisa mifugo (live stock officer), Afisa
utafiti mifugo
(livestock
research officer), Afisa Utumishi (human resources officer), Afisa ardhi
msaidizi,
Dereva
(driver).
Nafasi
nyingine ni pamoja na Afisa utalii, Afisa ushirika (cooperative officer), Afisa
Serikali za
mitaa
(local government officer) Mhandisi ufundi (mechanical engineer), Mhandisi
haidrojiolojia
(hydrogeologists),
Mhandisi (maji) – water resource engineer, Mhandisi (maji) – water resource
with
gis engineer, Mhandisi (umeme) Mhandisi mazingira (environmental engineer),
Mhandisi
kilimo
(agro – engineers), Afisa kilimo (agro – officers), Mkufunzi kilimo
(aquaculture), Afisa
kilimo
msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary
officers), Daktari utafiti
mifugo
(veterinary research officer).
Kada
nyingine ni Daktari mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo (animal
science),
Afisa
mifugo (live stock officer), Afisa utafiti mifugo (livestock research officer),
Afisa ardhi
msaidizi,
Afisa utalii, Afisa ushirika (cooperative officer), Ufundi (technician
mechanics), Fundi
sanifu
- ufundi (technician mechanics), Fundi sanifu - umeme (technician electrical),
Fundi
sanifu
– (water works technician), Fundi sanifu maabara– (water laboratory
technician), Fundi
sanifu
- maji - (technician- water),Fundi sanifu msaidizi (ufundi bomba) - (assistant
water works
technician
plumbing).
Wengine
ni Fundi sanifu msaidizi (upimaji ardhi) - (assistant water works technician
geometric),
Fundi
sanifu msaidizi mitambo ya maji (pampu),Fundi sanifu msaidizi mitambo ya maji
(umeme),
fundi sanifu msaidizi - (assistant technician welding), Mhandisi - ujenzi
(engineer–
civil),
Fundi sanifu – ramani (technician - (mapping) na Mpiga chapa msaidizi
(assistant printer)
.
Kwa
upande wa Tangazo la Kingereza kazi zilizotangazwa ni pamoja na "Senior
research
engineer",
"Research engineer assistant", "Principal engineer",
"Engineer", "Artisan", "Chief
accountant",
"Human resource development and administrative manager", "Human
resource
development
and administrative officer", "Welder", "Tutor",
"Principal planning and promotion
1
/ 2
SERIKALI
YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,324
officer",
"Director of planning, finance and administration", "Tutors
(travel & tourism), "Supplies
officer",
"Mediator", "Arbitrator", "State attorney",
"Personal secretary"," Office assistant",
"Security
guard", "Receptionist", "Transport officer", "Law
secretary", "Computer system
analyst",
"Librarian assistants", "Procurement specialist",
"Director of nutrition policy and
planning",
"Assistant medical officer", "Director of finance and
administration", "Environmental
management
officer-science".
Daudi
alifafanua kuwa nafasi hizo za kazi zilizo kwenye katika tangazo la lugha ya
Kiswahili ni
kwa
ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu
Mkuu
Wizara
ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu
Wizara
ya
Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu
Mwanasheria
Mkuu
wa Serikali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Shinyanga, Dodoma, Kilimanjaro,
Dar es
Salaam
na Rukwa, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Sikonge,
Liwale,
Handeni,
Iramba, Sumbawanga,Iringa, Tanga, Ileje, Korogwe pamoja na Mamlaka za Serikali
za
Mitaa.
Aliongeza
kuwa kwa tangazo la kazi la lugha ya Kiingereza waajiri wake ni pamoja na
Mamlaka
na
Bodi zifuatazo;- Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization
(TEMDO),
Tanzania
Automotive Technology Centre (TATC), Ardhi Institute Morogoro, Tea Board of
Tanzania
(TBT), National College of Tourism (NCT), The Commission for Mediation and
Arbitration
(CMA), Attorney General’s Chambers, Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC),
Kilimanjaro
Christian Medical Centre (KCMC), The National Environment Management council
(NEMC)
and The Cashewnut Board of Tanzania.
Katibu
amesema Utumishi wa Umma unahitaji watu makini, wenye weledi katika taaluma zao
na
wenye maadili mema, kwa kuwa mtumishi wa umma ni kioo cha jamii anaetakiwa
kufanya
kazi
kwa bidii ili kuiwezesha Serikali kutimiza malengo yake kwa ufanisi, ndio
sababu ofisi yake
inasisitiza
waombaji wa kazi kujiandaa vizuri ili kuweza kushindana na wengine wenye uwezo
kama
wao. Hivyo, amewataka waombaji wa nafasi za kazi kutembelea wao wenyewe tovuti
hiyo
ya
Sekretarieti ya Ajira ili kujua nafasi na daraja la kazi lililotangazwa ili
kuepuka uwezekano wa
kupewa
taarifa za kupotoshwa na kuomba kazi ambayo haijatangazwa na kujikuta mwombaji
akipoteza
fursa ya ajira bila ya sababu za msingi.
Mwisho
amebainisha kuwa mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi hizo zilizotangazwa
ni
tarehe 14 Julai, 2014 na kuwataka waombaji wote kuwasilisha maombi ya kazi kwa
njia ya
posta
kwa kutumia anwani iliyowekwa katika matangazo ya kazi.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniOfisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi
wa Umma. 30 Juni, 2014.
2
/ 2
No comments:
Post a Comment