Sio wengi wanaofahamu umuhimu wa kula samaki mara kwa mara na jinsi kitoweo hiki kilivyo na umuhimu pekee ktk afya ya binaadam,samaki ni kitoweo ambacho watu wengi hukiona cha kawaida sana.
Samaki inamafuta ambayo yanakiambatana cha OMEGA 3 yanayomfanya binaadamu kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri,kutunza kumbukumbu .. lkn pia mafuta hayo ndio pekee huzuia tatizo la ugonjwa wa moyo kama moyo kwenda mbio hata kama unataka mtoto wako awe na uwezo mzuri shuleni muwekee tabia ya kula samaki pia wamama wajawazito wanashauriwa sana kula samaki ili kuwajengea watoto wao uwezo mzuri wakiwa tumboni.
anaekula samaki mara 2 au mara 4 kwa wiki anapunguza 27% ya kupata kiharusi,zaidi ya mara tano kwa hupunguza 52% ya kupata kiharusi.
Faida nyingine za samaki
•Huyeyusha damu ma kuifanya iwe nyepesi
• Huilinda mishipa ya damu isiharibike
• Huzuia damu kuganda
• Hushusha shinikizo la damu
• Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi
• Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso
• Husaidia kuzuia uvumbe mwilini
• Huendesha mfumo wa kinga ya mwili
• Huzuia saratani
• Hutoa ahueni kwa wenye pumu
• Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo
• Huongeza nishati ya ubongo
Ni vyema kula sana samaki kuliko nyama nyekundu
Ni kitu kidogo lkn chenye faida kubwa